Dunia Ina Mema Mengi
***
Na
James |Kemoli Amata
***
Vitabu vya kawaida vya mwandishi huyu
Highly Regretted: An autobiography of a bad teacher, AuthorHouse, 2010
Kisa cha Zahara Mage (a novel in Swahili), Mvule Africa, 2008
Mtaala wa Fasihi kwa Shule za Sekondari (Curriculum of Literature for Secondary Schools), Igudwa, 2008
Taaluma ya Ushairi (Analysis of poetry in Swahili), Acacia, 2001
Makosa Katika Insha kwa Shule za Upili, ZC, 1999
Muhtasari wa Tungo na Insha, ZC, 2000
Insha: Usiteleze Katika Mtihani, ZC, 2000
Avasali vi Kivi (Intercessors of Calamity in Maragoli), Igudwa, 2003
Mwongozo wa Kipekee wa Mwisho wa Kosa, Africawide Network, 2005
Mwongozo wa Kipekee wa Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine, Africawide Network, 2005
Mwongozo wa Kipekee wa Kifo Kisimani, Africawide Network, 2005
Mwongozo wa Kipekee wa Utengano, Africawide Network, 2008
***
Vitabu vingine vya mtandao, ‘e-books’
Before and After Your Wedding
Keep on scratching! Or change by choice
Obesity and Poor Health
Ushairi na Aina na Bahari za Mashairi
Mitihani kielelezo ya Kiswahili KCSE
Life is Health and Wealth
Relax, Doctor
Mashairi Rahisi: Mazoezi na majibu
An Introduction To The Theory And Practice OfNetwork Marketing
Nelson Mandela Madiba
A villa for Zahara
Bahati alikata kiu
Don’t Wait For The Government
***
Dunia Ina Mema Mengi
(The World Is Full Of Goodness)
***
Toleo La Smashwords
***
Dunia Ina Mema Mengi
(Swahili for The World Is Full Of Goodness)
Hakimiliki © Oktoba, 2010 by James |Kemoli Amata
Anwani ya mahali:
Tianshi Specialty Shop
KVDA Plaza, Mezzanine Floor,
Eldoret
Kenya
Anwani ya posta:
Po Box 2-30105
Soy
Kenya
Rununu: +254 721 720 699/+254 734 720 699
Kipepesi: kemoli2003@yahoo.com
Watu wengi wameiba kazi zangu.
Usiwaige.
Kwa mujibu wa maadili, wajibu na sheria, haki zote ni za mwandishi.
***
(Toleo La Smashwords, Maelezo Ya Idhini
Hiki kitabu cha elektoniki kimeidhinishwa kwa minajili ya raha yako ya kibinafsi peke. Hiki kitabu kisiuzwe tena wala kisipewe watu wengine. Iwapo ungependa kukitumia hiki kitabu na mtu mwingine, tafadhali nunua nakala ya ziada kwa kila mpokezi. Iwapo unakisoma hiki kitabu na hukukinunua, au hakikununuliwa kwa minajili ya matumizi yako peke yako, basi tafadhali kirudishe kwa Smashwords.com na ununue nakala yako. Asante kwa kuiheshimu kazi ngumu ya mwandishi huyu.)
Smashwords Edition, License Notes
This ebook is licensed for your personal enjoyment only. This ebook may not be re-sold or given away to other people. If you would like to share this book with another person, please purchase an additional copy for each recipient. If you’re reading this book and did not purchase it, or it was not purchased for your use only, then please return to Smashwords.com and purchase your own copy. Thank you for respecting the hard work of this author.
***
Kimetangazwa Kwanza Na:
James Kemoli Amata katika Smashwords, Januari 2012
***
Mtabaruku
Mke wangu Margaret M’mbone
Na wajukuu wangu: Rachami, Kemoli, Savane, Ng’onyere, Walegwa na M’mbone.
***
Shukrani
Napenda nimshukuru sana Jennifer Chepkirui Lihasi
Wa Modern Professional Centre, Soy,
kwa kunipigia chapa msuada wa kitabu hiki.
Siwezi kusahau kutoa shurani za dhati kwa makala ya wavuti ya Steele Writers Nesletter nitumiwayo kila wiki kwa kipepesi kwa mafunzo na kunijulisha kuhusu Smashwords.com. Nasema asante sana.
Kabla niifikie tamati ya shukrani zangu, ni muhimu sana niishukuru Smashwords.com kwa kukubali kukitangaza kitabu hiki kama baadhi ya vitabu vya mtandao. Natarajia kuona tofauti katika juhudi zangu za uandishi.
***
Nukuu
‘Hayo yote ni ya dunia natambua, si ajabu yalonifika natambua…’
- Mike Enoch wa Dar es Salaam Jazz Band
***
Yaliyomo
Sura ya 1: Neno La Mungu
Sura ya 2: Watu Wakarimu
Sura ya 3: Vicheko
Sura ya 4: Warembo
Sura ya 5: Viumbe Na Maumbile
Sura ya 6: Vitu Vizuri
Sura ya 8: Mapenzi Na Mvuto
Sura ya 8: Duniani Mema Yamefurika
***
Dunia Ina Mema Mengi
***
Sura ya 1
Neno La Mungu
MAHALI papo. Papo mahali. Mahali papo katika maandiko matakatifu panapoonyesha uchungu huzaa dhana. Dhana yaweza kuwa ya ukweli au ya uongo. Mathayo Mtakatifu ana maneno. Ni maneno makali mno. Maneno haya ukiyasoma kwa makini, ni desturi yakugonge moyo. Mlango wa ishirini na saba, mstari wa arobaini na sita una maneno. Na kama saa tisa, Yesu akapasa sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama Sabakathani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Yasome maneno hayo tena. Maneno hayo yasome tena. Tena yasome maneno hayo. Hayo maneno yasome tena. Utahuzunika. Utasikitika.
Yesu, Mwana wa Mungu, alikuwa katika uchungu mkali, mkali, mkali sana. Mpaka akayatamka maneno haya ya kukatisha tamaa. Ni maneno ya kutamausha.
Tunataka maneno ya kuhamasisha. Mbona maneno ya kutamausha ndiyo yanayoyajaza masikio.
Maneno ya kutamausha yalianza zamani. Mwimbaji wa Zaburi ana nini? Ana mambo mengi sana. Katika mlango wa ishirini na mbili, Daudi mwana wa Yese alilia. Akiyatoa machungu aliyokuwa nayo aliongea. Mstari wa kwanza una maneno hayo ya kutamausha. Anasema:
Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?
Mungu hawaachi wapenzi wake. Mungu alimpenda Daudi. Mungu alimpenda Yesu. Mungu anawapenda Daudi na Yesu. Na ukumbuke Daudi na Yesu ni watu wa ukoo mmoja, jamaa, kwa mujibu wa fikira na vipimo vya wanadamu.
Hayo ni mambo aliyoyapitia Yakobo. Alikuwa amekaa sebuleni akisikiliza redio. Ulikuwa wakati wa kipindi cha Zilipendwa. Zilipendwa ni kipindi cha nyimbo zilizokuwa maarufu, zilizoshamiri miaka ya nyuma, siku za wazee, vijana wa siku hizo. Kipindi hicho hakikuwahi kumpita Yakobo. Kila Jumamosi, kwa redio yake ya transista alihamia Tanzania kwa kusikiliza Tanzania Broadcasting Corporation. Ingawa alikuwa Likuyani ama Wangulu kimwili alikuwa Tanzania, Dar es Salaam kiroho.
Jumamosi moja akasikia wimbo uliokuwa na maneno:
Humu Duniani, ‘hakuna’ kizuri,
Lililobaki ni kuvumilia.
Yakobo aliyakataa maneno hayo. Aliyaona kuwa ya uongo. Yalikuwa maneno ya kudanganya.
Jumamosi iyo hiyo alipata fursa ya kuusikiliza wimbo mwingine ulioshamiri siku za ujana mbichi wake. Aliuona kuwa upuuzi mwingine. Wimbo ulikuwa na maneno:
Dunia haina wema,
Tenda mema wende zako, na Mola atakulipia.
‘Kweli?’ Yakobo alijiuliza huku akitikisa kichwa, ishara ya kukataa.
Yaani, tangu zamani Dunia imetiwa dhana ya kuiona ina ubaya, uovu peke yake. Wanadamu wanaipaka tope Dunia. Imetiwa dhana ya kuiona ina ubaya, uovu peke yake. Wanadamu wanaipaka tope Dunia.
Wanadamu wao hao wanaosema ni wabaya na kwamba wao hukashifiwa mototo wa nyoka ni nyoka. Mwandamu ni mwanadamu. Lakini Mungu alimuumba mwanadamu vizuri. Alimuumba kwa umbo lake. Umbo la Mungu ni zuri. Mungu alipomuumba mwandamu alimwona kuwa mzuri sana. Akampendeza sana. Alimpendeza kabisa. Fikira za kumwona mwandamu kuwa mbaya zinawafanya watu wawaone watu kuwa wabaya. Lakini tukiwawazia watu uzuri tutaona watu ni wazuri. Tutawaona watu wazuri. Tutaona vitu vizuri. Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu ni mzuri. Mwanadamu ni mzuri.
Maneno ya kuikashifu Dunia yalikuwa katika maongezi ya watu mbali na kuwekwa katika nyimbo. Mahali pengi wanadamu walidai Dunia ni mbaya. Wengine wakawa daima wanadai Dunia imeharibika.
Shutuma dhidi ya Dunia zilimwuma na kumkera sana Yakobo. Alijitahidi sana kujizuia kutapika. Hata hivyo aliumwa kichwa kila aliposikia watu wakiilaumu Dunia kwa matendo ya watu. Kila mtu alipotenda tendo la ajabu, la kutoaminika, watu walimaka na kudai, ‘Dunia imeharibika kiasi cha kutorekebika.’
‘Yawezekana nilipo pawe pameharibika?’ Yakobo alijiuliza. ‘Na kama hapa pameharibika, hapa ni Dunia? Mbona paitwe Dunia?’
Kutaka kujua ukweli wa mambo kulimfungisha Yakobo safari ya kwenda mashariki.
Kituo chake cha kwanza kilikuwa Mung’oma. Huko alimpata mzee mmoja wa zamani sana akamwuliza swali lake la kwanza: ‘Dunia ni nini?’